Baraza linawatangazia Wanataaluma wake uwepo wa fursa ya mafunzo kwa njia ya mtandao yatakayotolewa na chuo cha Korea Health Industry Development Institute (KHIDI).
Chuo hiki ambacho kiko chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea (MoHWK) kitatoa mafunzo yajulikanayo kama Medical Korea Academy Online Training Program, MKA e-class. Mafunzo haya yanatarajiwa kuwapa washiriki ujuzi wa kitabibu na kuongeza au kukuza taaluma yao.
Kwa Wanataaluma wenye sifa na watakaopenda kushiriki mafunzo haya wanatakiwa kujisajili kupitia tovuti ya https://MKA-eclass.or.kr kuanzia tarehe 01 Juni mpaka 31 Julai 2024 na kuanzia tarehe 01 Septemba mpaka 31 Oktoba 2024. Mara baada ya usajili mshiriki anaweza kuanza mafunzo mara moja ndani ya tarehe tajwa hapo juu.